MTOKO Designs ni label ya mavazi (mitindo) ambayo inafanyakazi chini ya mwamvuli wa Youth Awareness Association (YAA).
MTOKO ni neno la Kiswahili lenye maana nyingi ingawa neno hili halipo katika Kiswahili fasaha lakini bado ni neno ambalo linatumika sana katika mazungumzo yetu ya kila siku likiwa na maana tofauti tofauti.
Kwetu sisi (MTOKO Designs) neno hili MTOKO limebeba maana takribani mbili;
1. Tukiwa kama vijana ambao tunaanza safari ya maisha yetu, MTOKO designs ndio kitu kinachotutoa/ kitachotutoa sisi vijana, kwani MTOKO designs imedhamiria kufanyakazi na vijana mbalimbali katika nyanja tofauti za fashion ili vijana tuweze kujiajiri.
2. Hali ya kupendeza katika vazi flani rasmi.Nauhakika hii tumesha kutana nayo sana mitaani pindi tunapokuwa tumependeza mtu hukusifia kwakuambia umetoka sana! Kwa maana kwamba umependeza sana. Hapa ndipo MTOKO designs huchukua nafasi yake.
LAKINI pia MTOKO designs imechukua taswira nzima ya mtembezi maalum, au wenzetu huita “OUTING”, lakini kwa lugha ya walio wengi hapa nyumbani huita MTOKO. Mtoko ni matembezi yalio maalum kwasababu maalum, mfano; Unaweza ukawa MTOKO kwa ajili ya party, unaweza ukawa MTOKO kwa ajili ya hata chakula cha usiku na kadhalika. Ili kufanikisha hii, MTOKO designs inaingia ili kuufanya MTOKO wako uwe wa uhakika kwa kukupatia MITOKO itayoendana na MTOKO wako.
MTOKO designs hasa ni kwa ajili ya kijana wa kisasa anaejijari na kuthamini uafrika wake, ndio maana tunajitahidi kutumia materials za kiafrika kama khanga, vitenge, batiki, masai na kadhalika ili kumfanya akubalike kokote aendapo kwa product zenye kubeba uhalisia wake, PROUDLY AFRICAN YOUTH.
Mpaka sasa mtoko imeshafanyakazi na watu mbalimbali ikiwa pamoja na waigizaji mbalimbali wa filamu, wanamuziki na watangazaji mbalimbalin wa vituo mbalimbali vya TV nchini. Pia tegemea mengi kuhusu MTOKO hivi karibuni.
Support MTOKO, ili vijana tutoke. MTOKO DESIGNS, PRODLY AFRICAN YOUTH.
No comments:
Post a Comment